728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 22, 2015

    MSIMBAZI KUNA MAMBO:USIMUITE KIIZA,NI SERGIO AGUERO

    BAADA ya mshambuliaji wa Simba, Mganda Hamis Kiiza kuifungia timu yake hiyo mabao matatu (hat-trick) katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi, mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi hao wameamua kumpachika jina la Sergio Aguero.

    Jina hilo ni la straika hatari wa Manchester City ya England, raia wa Argentina, Sergio Aguero ambaye ametokea kuwa moto wa kuotea mbali katika kucheka na nyavu.

    Kupachikwa jina hilo kwa Kiiza hakukuja hivi hivi bali ni kutokana na kuonyesha umahiri mkubwa katika kufunga mabao, akiwa amefanya hivyo katika mechi zote tatu za kwanza za Ligi Kuu Bara akiwa na kikosi chake hicho kipya cha Simba.


    Mganda huyo alianza cheche zake katika mchezo wao wa kwanza tu dhidi ya African Sports alipofunga bao pekee na la ushindi wa 1-0 kwa timu yake kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kabla ya kupiga moja tena walipocheza na Mgambo Shooting kwenye uwanja huo waliposhinda 2-0. 


    Wakati wapinzani wa mchezaji huyo na Simba kwa ujumla wakimbeza kuwa alibahatisha mabao yake hayo, juzi Jumapili aliwajibu kwa vitendo baada ya kupiga ‘hat-trick’ yake hiyo ya kwanza msimu huu, katika ushindi wa ambao 3-1 dhidi ya ‘Wakata Miwa’ hao wa mkoani Kagera.


    Ni kutokana na mabao yake hayo matano ndani ya mechi tatu, baada ya mchezo wa juzi mashabiki wa Simba walimshangilia mno Kiiza wakimwita kwa jina la Sergio Aguero, wakionyesha kumkubali kwa alichokifanya siku hiyo.


    Kwa kufikisha mabao matano, Kiiza amefanikiwa kuwafunika washambuliaji wenzake kama Donald Ngoma na Amissi Tambwe wa Yanga wenye mabao matatu kila mmoja.


    Kuelekea mchezo wa Jumamosi baina ya watani hao wa jadi, Kiiza anapewa nafasi kubwa ya kucheka na nyavu kutokana na kujiweka sawa kisaikolojia kutokana na kasi yake ya ufungaji mabao kwenye ligi hiyo.(Bingwa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MSIMBAZI KUNA MAMBO:USIMUITE KIIZA,NI SERGIO AGUERO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top