Daktari wa klabu ya Chelsea ya
nchini England Eva Carneiro ameamua kuondoka katika klabu hiyo wiki sita
baada ya kukwaruzana na meneja wa timu Jose Mourinho.
Carneiro
aliingiliwa katika majukumu yake baada ya Mourinho kusema kuwa benchi
lake la matibabu lilikuwa na watu wasiojua majukumu yao kwa kumtibu
hovyo Eden Hazard wakati wa sare ya 2-2 na Swansea tarehe 8 Agosti.
Chelsea
ilimuomba Carneiro mwenye miaka 42 kurejea kazini lakini alikataa na
kwa sasa analishughulikia suala hilo kisheria zaidi.
Chama cha Soka nchini humo FA kinafuatilia malalamiko kwamba Mourinho alitumia lugha ya matusi au kijinsia juu yake.
Chelsea wanasema hawana maoni juu ya masuala ya ndani ya Utumishi.
Mwenyekiti
wa Ushirikishwaji wa Bodi ya Ushauri ya FA Heather Rabbatts, ameelezea
kusikitishwa kwake juu ya kuondoka kwa Carneiro.
0 comments:
Post a Comment