728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 25, 2015

    MASHABIKI 10 ARSENAL MBARONI KWA KUHARIBU UWANJA


    London,England.

    Hivi umeshawahi kufuatilia uhasama uliopo kati ya vilabu vya Arsenal na Tottenham?Unajua mabalaa ya mashabiki wao?

    Sikia hii!!Juzi jumatano katika mchezo wa kombe la Capital One uliopigwa nyumbani kwa Tottenham White Hart Lane mashabiki wakorofi wa Arsenal wapatao kumi walitiwa nguvuni/mbaroni na askari baada ya kufanya fujo na kusababisha uharibifu wa vitu mbalimbali katika uwanja huo.

    Baadhi ya vitu vilivyoharibiwa na mashabiki hao walioshindwa kuzuia hisia zao kufuatia klabu yao kuibuka na ushindi wa bao 2-1 ni mabango ya matangazo ya biashara pamoja na bango lenye kauli mbiu ya klabu ya Tottenham lisemalo "This is my Club".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MASHABIKI 10 ARSENAL MBARONI KWA KUHARIBU UWANJA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top