Ndola,Zambia.
ZESCO United ya Mtanzania,Juma Ndanda Liuzio,imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Levy Mwanawasa ulioko Ndola baada ya jioni ya leo kuichapa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu finali ya klabu bingwa Afrika.
Shujaa wa Zesco United katika mchezo wa leo alikuwa ni Jackson Mwanza aliyefunga mabao yote mawili katika dakika za 55 na 57.Bao la kufutia machozi la Mamelodi Sundowns limefungwa na Zimbabwe Khama Billiat dakika ya 87.
Timu hizo zitarudiana tena Jumamosi Septemba 24 huko Johanesburg,Afrika Kusini,na mshindi ataumana na mshindi kati ya Zamalek ya Misri ama Wydad Casablanca ya Morocco katika mchezo wa fainali.
0 comments:
Post a Comment