YANGA SC imeonyesha kuwa ina dhamira ya dhati ya kuutetea ubingwa wake iliyoutwaa msimu uliopita baada ya jioni ya leo kuichapa Mwadui FC kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Amissi Tambwe SC alianza kuifungia Yanga SC la kuongoza dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza akimalizia pasi ya kichwa kutoka kwa Deus Kaseke.Bao hilo lilidumu mpaka wakati wa mapumziko.
Bao la pili la Yanga SC limefungwa na Mzimbambwe Donald Ngoma dakika ya 90 kwa kichwa akimalizia krosi safi ya Haruna Niyonzima toka wingi ya kulia.
Ushindi huo umeifanya Yanga SC kufikisha alama 10 baada ya kushuka dimbani mara nne.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliochezwa katika uwanja wa Uhuru,Dar Es Salaam,Simba SC imeifunga Azam FC 1-0.Shukrani kwa bao la dakika ya 67 la Shiza Kichuya
MATOKEO MENGINE
Majimaji 0-1 Ndanda FC
Ruvu Shooting 1-4 Mbao FC
Prisons 0-0 Mbeya City
Mtibwa Sugar 2-0 Kagera Sugar
0 comments:
Post a Comment