728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 28, 2016

    MESUT OZIL AKUBALI KANDARASI MPYA ARSENAL KWA MASHARTI MAKUBWA MAWILI


    London, Uingereza.

    KIUNGO wa Ujerumani ,Mesut Ozil,ameripotiwa kukubali kusaini kandarasi mpya ya miaka mitatu ya kuendelea kuitumikia klabu yake ya Arsenal.

    Mbali ya kuongeza kandarasi hiyo mpya itakayomweka Arsenal mpaka 2021 pia Ozil,27,ameboreshewa mshahara wake kutoka £140,000 kwa wiki mpaka £230,000 kwa wiki na kuwa mchezaji wa kwanza wa klabu hiyo kuvuka mshahara wa £200,000 kwa wiki.

    Wakati huohuo taarifa zaidi kutoka Bild zinasema Ozil amesaini kandarasi hiyo baada ya Arsenal kukubali masharti mawili makubwa aliyoyatoa ili aendelee kubaki Emirates.

    Sharti la kwanza lilikuwa ni kuachana na jezi Namba 11 na kupewa jezi Namba 10 ambayo hapo awali ilikuwa ikivaliwa na Jack Wilshere ambaye kwa sasa yuko FC Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.

    Sharti la pili lilikuwa ni Arsenal kuboresha kikosi chake kwa kununua wachezaji mahiri ili iweze kutwaa ubingwa wa ligi kuu England ambao imeupoteza kwa zaidi ya misimu kumi na mbili iliyopita.Kandarasi ya sasa ya Ozil inaisha mwaka 2018.

    Aidha baada ya kufanikiwa kumsainisha Ozil kandarasi hiyo mpya Arsenal pia imeripotiwa kuongeza kasi katika mazungumzo ya kumshawishi nyota mwingine wa klabu hiyo Alexis Sanchez nae akubali kusaini kandarasi mpya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MESUT OZIL AKUBALI KANDARASI MPYA ARSENAL KWA MASHARTI MAKUBWA MAWILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top