London,Uingereza.
CHAMA cha soka cha England (FA) kimemtimua kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo,Sam Allardyce,baada ya kumkuta na hatia ya kutumia vibaya madaraka yake.
Allardyce mwenye umri wa miaka 61 ameondolewa katika kiti chake hicho baada ya gazeti la Daily Telegraph kuripoti kuwa kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Bolton Wanderers,West Ham United na Sunderland alitumia vibaya cheo chake na kujipatia hongo ya Paundi 400,000 zilizotokana na kutoa ushauri mbaya ambao ulilenga kuzunguka/kuvunja sheria za uhamisho wa wachezaji katika dirisha lililopita la usajili.
Allardyce anaiacha England akiwa ameiongoza kucheza mchezo mmoja pekee uliokuwa wa kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.Katika mchezo huo England iliibuka kidedea kwa kuichapa Slovakia kwa bao 1-0 lililofungwa na Adam Lallana.
Nafasi ya Allardyce,itakaliwa kwa muda na Gareth Southgate kama kocha wa muda mpaka hapo kocha mpya atakapopatikana.
0 comments:
Post a Comment