728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 21, 2016

    WAKALA WA YAYA TOURE AMTUPIA DONGO GUARDIOLA,ASEMA HATA BABU YAKE ANGETWAA UBINGWA BARCA,BAYERN


    Manchester, Uingereza.

    WAKALA wa Yaya Toure,Mrusi Dimitri Seluk,amemtupia dongo kocha wa Manchester City,Mhispania Pep Guardiola na kusema kuwa kocha huyo siyo bora kama wengi wanavyodhani bali amekuwa akifanikiwa kutokana na jasho la watu wengine.

    Kauli hiyo ya Seluk imekuja muda mfupi baada ya Guardiola kudai kuwa Toure hataichezea tena Manchester City mpaka hapo wakala huyo atakapomwomba msamaha kutokana na kumtolea maneno makali pale alipomwengua mteja wake katika kikosi cha Manchester City cha ligi ya mabingwa Ulaya.




    Seluk akifanya mahojiano mtandao wa The Mirror amesema amesema Pep siyo bora kama wengi wanavyodhani.Hata mafanikio ambayo amekuwa akiyapata yamekuwa yakitokana na jasho la watu wengine na siyo kwa jasho lake na juhudi zake.

    Amesema "Pep alifanikiwa akiwa Barcelona na Bayern Munich,lakini hebu tazama nyuma ya mafanikio hayo.

    "Timu aliyokuwa nayo Barcelona ilikuwa tayari imejengwa na mtangulizi wake Frank Rijkaard na pia alikuwa na bahati kuwa na Lionel Messi kikosini.Messi ndiye aliyeibeba Barcelona na siyo Pep.Luis Enrique ameonyesha kwamba mafanikio ya Barcelona hayakutokana na Pep.

    Hivyo hivyo hata Munich. Bayern Munich walikuwa wametwaa mataji matatu kabla ya ujio wa Pep.Tayari walikuwa na timu nzuri ndani na nje ya uwanja.Asingeweza kushindwa [Kufeli] hata babu yangu angetwaa mataji na timu kama hiyo.

    Wakati huohuo Seluk amesema atamwomba msamaha Guardiola ikiwa na yeye atamwomba msamaha mteja wake Yaya Toure na pia kama atawaomba msamaha Joe Hart na Manuel Pellegrini kwa yote aliyowatendea.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAKALA WA YAYA TOURE AMTUPIA DONGO GUARDIOLA,ASEMA HATA BABU YAKE ANGETWAA UBINGWA BARCA,BAYERN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top