728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 30, 2016

    SAMATTA ATOKEA BENCHI GENK IKIPATA USHINDI WA KWANZA EUROPA LIGI

    Genk,Ubelgiji.

    KRC GENK inayochezewa na Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Ally Samatta,imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya ligi ndogo ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi baada ya Alhamis usiku kuichapa klabu ngumu ya Sassuolo ya Italia kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa kundi F uliochezwa katika uwanja wa Cristal Arena ulioko katika mji wa Genk.



    Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi Liany kutoka Israel,ilishuhudiwa Mbwana Samatta akiingia uwanjani dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Nikos Karelis na kuikuta KRC Genk ikiwa tayari inaongoza kwa mabao hayo 3-1 yaliyofungwa na Nikos Karelis 8',Leon Bailey 25',na Thomas Buffel 61'.Bao la Sassuolo limefungwa na Matteo Politano 65'. 

    Huo ni ushindi wa kwanza kwa KRC Genk katika michuano hiyo kwani katika mchezo wake wa awali uliochezwa huko Austria, wiki mbili zilizopita ilichapwa mabao 3-2 na Rapid Wien.



    VIKOSI

    Genk: Bizot; Walsh, Brabec, Colley, Nastic;Pozuelo, Ndidi, Susic (Kumordzi 82); Bailey,Karelis (Samatta 75), Buffel (Trossard 87)

    Sassuolo: Consigli; Lirola, Letschert, Acerbi,Peluso; Biondini (Ragusa 59), Magnanelli,Pellegrini (Mazzitelli 66); Ricci (Caputo 79),Defrel, Politano


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI GENK IKIPATA USHINDI WA KWANZA EUROPA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top