London, Uingereza.
DROO ya raundi/hatua ya 4 ya EFL CUP maarufu kama kombe la ligi imefanyika usiku huu baada ya michezo ya raundi/hatua ya 3 kukamilika.
Mahasimu Manchester United na Manchester City watakutana tena katika hatua hii.Mchezo ukiwa katika uwanja wa Old Trafford.
Westham United watakuwa wenyeji wa Chelsea huku Arsenal wakipangwa kukutana na timu ya daraja la kwanza ya Reading inayonolewa na beki wa zamani wa Manchester United,Jaap Stam.
Droo Kamili
West Ham vs Chelsea
Manchester United vs Manchester City
Arsenal vs Reading
Liverpool vs Tottenham
Bristol City vs Hull
Leeds vs Norwich
Newcastle United vs Preston
Southampton vs Sunderland
Michezo imepangwa kufanyika katika wiki ya Octoba 24,2016.
0 comments:
Post a Comment