728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 26, 2016

    ARSENAL YAJITOSA KWA YAYA TOURE MPYA


    London,Uingereza.

    ARSENAL imeripotiwa kuungana na vilabu vya Southampton,Schalke 04,Monaco na Roma katika mbio za kuisaka saini ya kiungo wa Atalanta ya Italia,Muivory Coast,Franck Kessie,ambaye kiuchezaji amekuwa akifananishwa na staa mwenzake wa nchi hiyo,Yaya Toure.

    Wakala wa Kessie,anayeitwa George Atangana ameuambia mtandao wa Goal.Com kuwa Arsenal imekuwa ikimfuatilia mteja wake kwa karibu zaidi na tayari msimu huu imeshatuma maskauti wake mara mbili kwenda kumtazama wakati akiichezea Atalanta.


    Aidha Atangana amesema licha ya Arsenal ya kuonyesha nia ya kumtaka Kessie,19,lakini italazimika kupambana sana kuipata saini ya kiungo huyo kwani kuna vilabu vingi vya ndani na nje ya Italia ambavyo vimeonyesha nia ya kuitaka Huduma yake.

    Kessie ambaye ameichezea Ivory Coast michezo minne mpaka sasa amekuwa kivutio kikubwa kwa vilabu vingi vya Ulaya baada ya msimu huu kuifungia Atalanta mabao manne katika michezo mitano ya ligi ya Seria A.

    Inasemekana msimu huu Kessie alikaribia kujiunga na Sunderland lakini kukosekana kwa kibaria cha kufanyia kazi nchini Uingereza kulikwamisha uhamisho huo.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YAJITOSA KWA YAYA TOURE MPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top