728x90 AdSpace

Thursday, September 22, 2016

HIKI NDICHO KIPINDI AMBACHO MESSI ATAKUWA NJE YA DIMBA BAADA YA KUUMIA



Barcelona,Hispania.

STAA wa Barcelona,Lionel Messi atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu hii ni baada ya jana Jumatano usiku kuumia katika mchezo wa ligi ya La Liga dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Katika mchezo huo Messi,29,alishindwa kumaliza dakika 90 baada ya kugongana na beki wa Atletico Madrid,Diego Godin na kisha kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Arda Turan dakika 59 ya kipindi cha pili.

Hii ina maana kwamba katika kipindi hicho cha wiki tatu Messi ataikosa michezo mitatu itakaoihusisha klabu yake ya Barcelona.

Michezo ni pamoja na ule wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani na michezo miwili ya ligi ya La Liga dhidi ya Sporting Gijon na Celta Vigo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: HIKI NDICHO KIPINDI AMBACHO MESSI ATAKUWA NJE YA DIMBA BAADA YA KUUMIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown