728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, September 28, 2016

    LECEISTER CITY USHINDI ASILIMIA 100 LIGI YA MABINGWA ULAYA NA REKODI JUU (+VIDEO)

    Leceister City,Uingereza.

    LECEISTER CITY imeendeleza moto wake katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya leo usiku kushinda mchezo wake wa pili mfululizo wa michuano hiyo kwa kuitungua FC Porto ya Ureno kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa kundi G uliochezwa katika uwanja wa King Power huko Leceister.

    Bao pekee na la ushindi katika mchezo huo limefungwa dakika ya 25 kwa kichwa na Mshambuliaji wa kimataifa wa Algeria Islam Slimani.

    Slimani mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu ya Leceister City amefunga bao hiyo akiunganisha krosi ya nyota mwenzie wa Algeria,Riyad Mahrez.

    Ushindi huo umeifanya Leceister City ifikishe pointi sita na kuongoza kundi G huku ikiwa imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya mtoano.

    REKODI

    Ushindi dhidi ya FC Porto umeifanya Leceister City kuwa klabu ya kwanza kutoka nchini Uingereza kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi ya mabingwa Ulaya ikiwa katika msimu wake wa kwanza katika michuano hiyo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LECEISTER CITY USHINDI ASILIMIA 100 LIGI YA MABINGWA ULAYA NA REKODI JUU (+VIDEO) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top