Montpellier,Ufaransa.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Benin, Stephane Sessegnon (Kulia) akitambulishwa baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia klabu ya Montpellier inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa.
Sessegnon,32,amejiunga na Montpellier akiwa kama mchezaji huru baada ya mwezi Mei mwaka huu kutemwa na klabu ya West Brom inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.
Vilabu vingine alivyowahi kuvichezea Sessegnon ni pamoja na Sunderland, Paris Saint-Germain na Le Mans.
Ikumbukwe dirisha la usajili kwa wachezaji huru barani Ulaya bado halijafungwa ndiyo bado baadhi ya vilabu vinaendelea kuimarisha vikosi vyao.
0 comments:
Post a Comment