Phelipe Coutinho ameibuka shujaa baada ya kuifungia goli la ushindi klabu yake ya Liverpool ilipovaana jioni hii na klabu ya Stoke City katika dimba la Britannia.
Coutinho amefunga goli hilo dakika ya 86 kwa shuti kali la mbali lililomzidi maarifa kipa wa Stoke City Butland na kujaa wavuni.Ushindi huo muhimu umeipoza kidogo Liverpool kwani katika mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu katika uwanja huo ilikubali kichapo cha goli 6-1.
0 comments:
Post a Comment