London,England.
Klabu ya Arsenal imeuanza vibaya msimu mpya wa ligi ya England baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa klabu ya Westham United katika mchezo mkali uliopigwa leo mchana katika uwanja wa Emirates.
Westham United ilipata goli lake la kwanza dakika ya 43 baada ya kiungo Cheikhou Kouyate kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Dimitri Payet huku goli la pili likifungwa dakika ya 57 na mshambuliaji Mauro Zarate baada ya kumpokonya mpira winga Alex Oxlade Chamberlain na kumfunga kirahisi kipa Peter Cech.
Baada ya magoli hayo Arsenal ilijitahidi kupambana ili kusawazisha magoli hayo lakini kikwazo kikubwa kilikuwa ni kipa wa Westham aitwaye Adrian ambaye alikuwa imara kuhakikisha haruhusu goli lolote.
Katika mchezo mwingine Newcastle imetoka sare ya goli 2-2 na Southampton.
0 comments:
Post a Comment