Dar Es Salaam,Tanzania.
SHIRIKISHO la Soka la Ulimwenguni (FIFA) limefungua mtandao wa usajili wa Kimataifa, ujulikanao kama Transfer Matching System (TMS) wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Ligi Daraja la Kwanza ili kutoa fursa kwa vilabu vya Yanga na Coastal Union kutuma usajili wao.
Hatua hiyo inafuatia ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa FIFA,baada ya Yanga SC na Coastal Union kuchelewa kutuma usajili wake katika siku ya mwisho ambayo ilikuwa ni Agosti 6,mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF ni kwamba dirisha la usajili la Bara limefunguliwa kwa saa 48 kuanzia leo Jumamosi na litafungwa Kesho Jumapili saa 6 usiku.
Wakati Yanga SC na Coastal Union wakichelewa kutuma usajili wao kwa wakati,Usajili wa vilabu vya Mashujaa,African Lyon,Kiluvya UnitedAbajalo FC,Kitayosa,Mvuvuma na Friends Rangers ulikutwa na kasoro.
0 comments:
Post a Comment