728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 23, 2016

    VUGUVUGU LA USAJILI ULAYA:MWINGINE AFELI VIPIMO AKIJARIBU KUHAMIA TIMU MPYA


    Kiryat,Israel.

    WAKATI dirisha la usajili barani Ulaya likiendelea kushika kasi,balaa la wachezaji kufeli vipimo kwa sababu mbalimbali nalo limeendelea kuwaandama kila inapoitwa leo. 

    Siku ya jana Jumanne bahati mbaya ilimuangukia Mshambuliaji wa Enyimba FC ya Nigeria,Christian Obiazor,baada ya uhamisho wake kwenda klabu ya Kiryat Shmona ya Israeli kukwama kufuatia kufeli vipimo vyake vya afya.

    Taarifa kutoka nchini Nigeria zinasema Enyimba ilikuwa imeshafikia makubaliano na Kiryat Shmona kumtoa Obiazor kwa mkopo wa msimu mmoja ambapo ingelipwa ada ya €50,000 kisha ingelipwa €100,000 kama ada ya kumnunua moja kwa moja.

    Sababa ya Obiazor kufeli vipimo imebainika kwamba nyota huyo aliyefanya vizuri kwenye michuano ya CHAN ya mwaka 2014 alikuwa na jeraha katika mguu wake wa kulia ambalo yeye na wakala wake Yomi Itshekure walijaribu kulifanya siri ili aweze kufanikisha uhamisho huo lakini vipimo vimewaumbua na Kryat Shmona imeamua kuachana nae.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VUGUVUGU LA USAJILI ULAYA:MWINGINE AFELI VIPIMO AKIJARIBU KUHAMIA TIMU MPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top