728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 28, 2016

    HATIMAYE SIMONE ZAZA ATUA WESTHAM UNITED


    London,Uingereza.

    KLABU ya Westham United maarufu kama The Hammers mchana huu imetangaza kumsajili Mshambuliaji wa kimataifa wa Italia,Simone Zaza,kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka klabu ya Juventus.

    Westham United imeipata saini ya Zaza baada ya kulipa ada ya mkopo ya €5m ili kupata haki ya kutumia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye msimu uliopita alifunga mabao matano katika michezo 19 na anaweza kujiunga moja kwa moja na klabu hiyo kwa ada ya €20m.




    Zaza anakuwa mchezaji wa 11 kujiunga na Westham United tangu dirisha la usajili lilipofunguliwa mapema mwezi Julai mwaka huu.

    Kabla ya kujiunga na Juventus,Zaza,aliwahi kuvichezea vilabu vya Atalanta, Sampdoria na Sassuolo na alikuwa sehemu ya kikosi cha Italia kilichoshiriki michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HATIMAYE SIMONE ZAZA ATUA WESTHAM UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top