728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 27, 2016

    VPL:SIMBA SC YAKALIWA KOONI NA RUVU JKT,AZAM FC,MWADUI SAFI


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    LICHA ya usajili wa nguvu iliyoufanya msimu huu,Simba SC,leo imeshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya kutofungana na maafande wa Ruvu JKT katika mchezo mkali wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa taifa,Dar Es Salaam.

    Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Azam FC ikiwa nyumbani Chamazi Complex imeibuka na ushindi mnono baada ya kuichapa Majimaji ya Songea kwa jumla ya mabao 3-0.

    Mbao FC ikiwa nyumbani CCM Kirumba imefungwa bao 1-0 na Mwadui FC ya Shinyanga.Mtibwa Sugar imeifunga Ndanda FC 2-1.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:SIMBA SC YAKALIWA KOONI NA RUVU JKT,AZAM FC,MWADUI SAFI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top