Milan,Italia.
Klabu ya Inter Milan imevipiga bao vilabu vya Manchester United na Real Madrid baada ya jioni hii kutangaza kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa Santos ya Brazil,Gabriel Barbosa Almeida maarufu kama Gabigol kwa ada ya £25milioni.
Gabigol mwenye umri wa miaka 20 amesaini mkataba wa miaka mitano utakaomuweka Milan mpaka mwaka 2021.
Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil kilichotwaa ubingwa wa michuano ya Olimpiki anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na Inter Milan baada ya Joao Mario aliyejiunga akitokea Sporting Lisbon ya Ureno.
0 comments:
Post a Comment