Hamis Kiiza
Bethlehem,Afrika Kusini.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa vilabu vya Yanga SC na Simba SC,Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ yupo katika hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Free State Stars inayoshiriki ligi kuu ya nchini Afrika Kusini maarufu kama ABSA Premiership.
Kiiza ambaye aliachwa na Simba SC msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania bara kwa madai ya utovu wa nidhamu amefuzu majaribio ya wiki moja katika klabu hiyo na atasaini mkataba wa mwaka mmoja mara tu atakapopata hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF).
Free State Stars ambayo ina makao yake makuu katika uwanja wa Goble Park inachezewa na Mtanzania,Mrisho Khalfani Ngasa.
0 comments:
Post a Comment