Coruna,Hispania.
ILE kiu ya mashabiki wa Arsenal kuona klabu yao kipenzi inasajili mshambuliaji mpya msimu huu huenda ikakoma hivi karibuni baada ya klabu hiyo kudaiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Deportivo de La Coruna,Lucas Perez kwa ada ya £17m.
Taarifa kutoka gazeti la michezo la nchini Hispania la El Confidential zinasema Arsenal imepewa nafasi ya kumsajili Perez mwenye umri wa miaka 27 baada ya kuvizidi ujanja dakika za mwisho vilabu vya Valencia na Everton.
Arsenal imeamua kumgeukia Perez anayetumia vyema mguu wa kushoto baada ya kushindwa kuwasajili washambuliaji Gonzalo Higuain,Mauro Icardi, Alvaro Morata, Jamie Vardy na Alexandre Lacazette
Msimu uliopita Perez alifungia Deportivo de La Coruna mabao 17 katika michezo 37 ya ligi ya La Liga.Msimu huu tayari ameshafunga bao moja katika mchezo mmoja.
VIDEO:
0 comments:
Post a Comment