Abidjan, Ivory Coast.
ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Al Ahly ya Misri rasmi zimetupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya jioni ya leo kushindwa kutambiana kufuatia kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa mwisho wa kuhitimisha michezo ya hatua ya nane bora.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Stade Robert Champroux huko Abidjan Ivory Coast licha ya timu zote kuonyesha soka safi lakini safu za ushambuliaji zilionekana kukosa umakini na kushindwa kutumia nafasi chache zilizopatikana.Katika mchezo wa awali uliochezwa huko Misri wiki kadhaa zilizopita Asec Mimosas ilishinda kwa mabao 2-1.
Matokeo hayo yamezifanya Al Ahly na Asec Mimosas kuishia katika hatua ya nane bora baada ya kujikusanyia alama sita na tano nyuma ya Wydad Casablanca na Zesco United zenye alama kumi na moja na alama tisa.
Katika mchezo mwingine kundi A uliochezwa huko Ndola,Zambia,Zesco United na Wydad Casablanca zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.Zote zimefuzu nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment