London, Uingereza.
MABAO mawili ya Mshambuliaji wa Ubelgiji, Michy Batshuayi,yameipa Chelsea ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Bristal Rovers katika mchezo mkali wa hatua ya nne ya michuano ya EFL (Kombe la Ligi) uliochezwa usiku huu katika uwanja wa Stamford Blidge.
Batshuayi alianza kuipa raha Chelsea baada ya kuifungia bao la kuongoza dakika ya 29 ya mchezo kabla ya dakika ya 31 Victor Moses kuongeza bao la pili.Bao la tatu la Chelsea limefungwa dakika ya 41 na Michy Batshuayi.
Mabao ya Bristal Rovers yamefungwa na Peter Hartley dakika ya 34 ya mchezo pamoja na Ellis Harrison aliyefunga bao la pili kwa mkwaju wa penati na kufanya mchezo uishe kwa Chelsea kutoka kifua mbele uwanjani kwa ushindi wa mabao 3-2.
Katika mchezo mwingine Liverpool ikiwa ugenini imechomoza na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Burton Albion shukrani kwa mabao ya Divock Origi,Roberto Firmino,Tom Naylor na Daniel Sturridge,aliyefunga mabao mawili.
Matokeo hayo yamezipeleka Chelsea na Liverpool hatua ya tatu ya michuano ya EFL
Matokeo Mengine ya EFL yako kama Ifuatavyo
Crystal Palace 2 - 0 Blackpool
Blackburn Rovers 3 - 3 Crewe Alexandra
Burton Albion 0 - 5 Liverpool
Chelsea 3 - 2 Bristol Rovers Derby County 1 - 1 Carlisle United
Everton 4 - 0 Yeovil Town
Exeter City 1 - 3 Hull City
Luton Town 0 - 1 Leeds United
Millwall 1 - 2 Nottingham Forest
Newcastle United 2 - 0 Cheltenham Town
Northampton Town 2 - 2 West Bromwich Albion
Norwich City 6 - 1 Coventry City
Oxford United 2 - 4 Brighton & Hove Albion
Peterborough United 1 - 3 Swansea City
Preston North End 2 - 0 Oldham Athletic
Queens Park Rangers 2 - 1 Rochdale
Scunthorpe United 1 - 1 Bristol City
Stevenage 0 - 4 Stoke City
Watford 1 - 1 Gillingham
Wolverhampton Wanderers Cambridge United
Reading 1 - 1 Milton Keynes.
0 comments:
Post a Comment