728x90 AdSpace

Wednesday, August 24, 2016

USAJILI MPYA EPL:JANMAAT AIKACHA NEWCASTLE UNITED NA KUJIUNGA NA WATFORD


Watford, Uingereza.

KLABU ya Watford imeendelea na harakati za kukiimarisha kikosi chake hii ni baada ya jioni ya leo kutangaza kukamilisha usajili wa mlinzi wa kulia wa Kidachi Daryl Janmaat kutoka Newcastle United kwa ada ya £7m.

Janmaat,27,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Watford na anatarajiwa kuanza kuichezea klabu hiyo Jumamosi ya wiki hii pale itakaposhuka dimbani kuvaana na Arsenal katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu Uingereza.

Janmaat alijiunga na Newcastle United mwaka 2014 kwa ada ya £5m akitokea Feyenoord ya nyumani kwao Uholanzi na kufanikiwa kuichezea michezo 78 akifunga mabao manne klabu ya klabu hiyo kushuka daraja msimu uliopita.

Janmaat anakuwa mchezaji wa nane kujiunga na Watford msimu huu baada ya Jerome Sinclair, Christian Kabasele, Isaac Success, Juan Camilo Zuniga, Brice Dja Djedje, Younes Kaboul na Roberto Pereyra.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: USAJILI MPYA EPL:JANMAAT AIKACHA NEWCASTLE UNITED NA KUJIUNGA NA WATFORD Rating: 5 Reviewed By: Unknown