728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 29, 2016

    SAM ALLARDYCE ATANGAZA KIKOSI CHAKE CHA KWANZA ENGLAND,AMTOSA RASHFORD,WILSHERE,AWAITA WALCOTT,ANTONIO

    London,England.

    MENEJA Mpya wa England Sam Allardyce jana kwa mara ya kwanza ametangaza kikosi chake tangu apewe mikoba ya kuinoa timu hiyo mapema mwezi Julai mwaka huu tayari kwa kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kuwemo kwenye fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.

    Katika kikosi hicho ambacho Septemba 4 kitakuwa ugenini Slovakia,Allardyce, amemuita kwa mara ya kwanza kiungo wa West Ham,Michail Antonio,huku pia akiwarejesha kikosini Danny Drinkwater na Theo Walcott ambao walikosa michuano ya Euro 2016.



    Michail Antonio

    Aidha Jack Wilshere,Ross Barkley na Marcus Rashford wameachwa kwa sababu mbalimbali huku beki wa kushoto wa Manchester United,Luke Shaw,akiitwa kwa mara ya kwanza tangu apone jeraha la kuvunjia mguu.

    KIKOSI KAMILI

    Makipa: Fraser Forster (Southampton),Joe Hart (Manchester City), Tom Heaton (Burnley)

    Mabeki: Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Phil Jagielka (Everton),Danny Rose (Tottenham Hotspur), Luke
    Shaw (Manchester United), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Manchester City), Kyle Walker (Tottenham Hotspur)

    Viungo: Dele Alli (Tottenham Hotspur),Michail Antonio (West Ham United), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool),
    Wayne Rooney (Manchester United),Raheem Sterling (Manchester City), Theo Walcott (Arsenal)

    Washambuliaji: Harry Kane (Tottenham Hotspur),Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City).

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAM ALLARDYCE ATANGAZA KIKOSI CHAKE CHA KWANZA ENGLAND,AMTOSA RASHFORD,WILSHERE,AWAITA WALCOTT,ANTONIO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top