728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 20, 2016

    SIMBA SC YAUANZA MSIMU MPYA KIBABE,YAICHAPA NDANDA FC 3-1 U/TAIFA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    SIMBA SC imeuanza kibabe msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo mkali ulioisha hivi punde katika Uwanja wa taifa,Dar Es Salaam.

    Laudit Mavugo alianza kuifungia Simba SC baada la kwanza dakika ya 19 ya mchezo akiunganisha mpira wa adhabu kutoka kwa Mohammed Hussein Tshabalala.

    Bao hilo halikudumu sana kwani dakika ya 36 Omary Mponda aliifungia Ndanda FC bao la kusawazisha kwa kichwa akiunganisha kona ya Kiggi Makassy na kufanya timu zote ziende mapumziko zikiwa sare.

    Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Simba SC Joseph Omog ya kumtoa Ibrahim Ajib na kumuingiza Fredrick Blagnon yalizaa matunda baada ya mshambuliaji huo wa Ivory Coast kufungwa kwa kichwa dakika ya 74.Bao la tatu la Simba SC limefungwa dakika ya 79 na Chiza Kichuya kwa mkwaju mkali wa mbali baada ya kuunasa mpira uliopanguliwa na kipa wa Ndanda FC,Jackson Chove.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA SC YAUANZA MSIMU MPYA KIBABE,YAICHAPA NDANDA FC 3-1 U/TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top