Milan,Italia.
INTER MILAN imeendelea na ujenzi wa kikosi chake hii ni baada ya leo mchana kutangaza kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ureno, Joao Mario,kutoka Sporting Lisbon kwa ada ya €45m.
Mario,23,ambaye mwezi Julai aliichezea Ureno michezo yote saba ya Euro 2016 amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia miamba hiyo ya jiji la Milan.
Usajili huo umemfanya Joao Mario aweke rekodi ya kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa pesa nyingi zaidi katika historia ya ligi kuu ya nchini Ureno.Awali rekodi hiyo ilishikiliwa na James Rodriguez baada ya kuhamia Monaco akitokea FC Porto
Joao Mario alijiunga na Sporting Lisbon akiwa na umri wa miaka11 akitokea katika shule ya soka ya klabu ya FC Porto na mchezo wake wa kwanza akiwa na Sporting Lisbon ulikuwa mwaka 2011 alipoingia uwanjani katika mchezo wa Europa Ligi dhidi ya Lazio.
0 comments:
Post a Comment