Mwanza,Tanzania.
TOTO Africans imeuanza vyema msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya jioni ya leo kuishushia Mwadui FC kichapo cha bao 1-0 katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza.
Bao la ushindi katika mchezo huo pekee wa ligi kuu Jumatano ya leo limefungwa dakika ya 36 na Mshambuliaji Waziri Junior Shentembo.
Hii ni mara ya tatu kwa Toto Africans kuitambia Mwadui FC katika michezo ya ufunguzi wa pazia la ligi kuu bara.
0 comments:
Post a Comment