Valencia,Hispania.
MIOYO ya mashabiki wa Arsenal huenda ikaendelea kuumia zaidi na zaidi katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya hii ni kutokana na klabu yao kuendelea kushindwa kufanya sajili zenye tija msimu huu.
Baada ya kushindwa kuwasajili Jamie Vardy,Gonzalo Higuani na Ryad Mahrez,Arsenal,inaelekea kwa mara nyingine tena kukwama kumsajili Mlinzi,Shokradi Mustafi,hii ni baada ya kocha wa Valencia,Pako Ayestaran,kusisitiza kuwa staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani hataihama klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili.
Kauli hiyo ya Ayestaran imekuja baada ya Jumatatu usiku kuishuhudia klabu yake ya Valencia ikiuanza vibaya msimu mpya wa La Liga kwa kufungwa mabao 4-2 na Las Palmas katika mchezo ambao Mustafi alianzia benchi na kuingia uwanjani matokeo yakiwa 3-1.
"Mustafi hauzwi,hataihama Valencia msimu huu.Ni mchezaji muhimu namhitaji katika kikosi changu".
Wakati huohuo taarifa kutoka nchini Hispania zinasema Valencia inaweza kurudi nyuma na kumuuza Mustafi ikiwa tu Arsenal itakubali kutoa kitita cha £43.1m kwa ajili ya kumsajili mlinzi huyo wa zamani wa Everton.
Mbali ya Mustafi,Valencia,pia imetangaza kuwa Mshambuliaji wake,Paco Alcacer,anayewindwa na Barcelona na yeye hataruhusiwa kuhama katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment