UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari
wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na
wengine wenye tabia za uzushi.
Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki
huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na
kumtamkia maneno yasiyostahili.
Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya
siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mah a k a - mani kutoa
ushahidi wa kile a l i - chokisema.
“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko,
tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa
akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.
Katika mahoj i a n o na kituo kimoja cha redio hivi karibuni Kessy
alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati
akiwa Mtibwa.
“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa
nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka
kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.
Manara alisema anashangazwa na mchezaji huyo badala ya kucheza mpira anazungumza taarab.
Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya
Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi
wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.
Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana
kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa
(FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na
Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.
Awali, Kamati hiyo ilisikiliza kesi hiyo na kumtaka Kessy kuilipa
Simba dola za Marekani 60, 000 lakini Simba walisema wanahitaji walipwe
dola 600,000 kama fidia ya kuvunja mkataba ikiwa ni kipengele ambacho
kipo kwen y e m k a t a b a kati yao kwa atakayevunja mkataba at
amlipa mwenziwe fedha hizo.
Simba inadai kuwa mchezaji huyo alisaini Yanga Juni 15 na kwamba ina
vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na mchezaji huyo kuvaa jezi za Yanga na
kusafiri na timu hiyo Uturuki kabla ya Juni 20 ambayo Yanga inadai ndio
siku iliyomsajili mchezaji huyo.
Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha
mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati
wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa
taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na
Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki
hii.
0 comments:
Post a Comment