Dar Es Salaam,Tanzania.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametaja kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya pambano la kukamilisha ratiba ya mechi za kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 nchini Gabon.
Katika kikosi hicho Kuna mabadiliko machache ukilinganisha na uteuzi uliopita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeruhi na kushuka kwa viwango.
Mshambuliaji Thomas Ulimwengu pamoja na beki wa kulia,Juma Abdul wameachwa kutokana na majeruhi.
Kiungo Mwinyi Kazimoto ametemwa na nafasi yake kuchukuliwa na chipukizi Muzamiru Yassin wa Simba.
Simon Msuva pia amerudishwa katika kikosi huku David Kaseke akitemwa.
Kikosi Kamili:
Makipa: Mlango: Deogratius Munishi, Aishi Manula.
Mabeki:Kelvin Yondani, David Mwantika,Vincent Andrew, Shomari Kapombe, Mwinyi Haji, Mohamed Hussein.
Viungo: Jonas Mkude, Himid Mao, Muzamiru Yassin, Shiza Ramadhan, Farid Mussa, Simon Msuva.
Washambuliaji: John Bocco, Mbwana Samatta, Ibrahim Hajib.
0 comments:
Post a Comment