Manchester, England.
Manchester City imetangaza kumsajili mlinda mlango Claudio Bravo kutoka FC Barcelona kwa ada ya £17m.
Bravo,33,amejiunga na Manchester City kwa mkataba wa miaka minne na anatarajiwa kushuka dimbani wikendi hii wakati klabu hiyo ya jiji la Manchester itakapokuwa ikipepetana na Westham United.
Bravo anakuwa mlinda mlango wa kwanza kutoka Chile kusajiliwa na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.
Bravo alijiunga na FC Barcelona mwaka 2014 akitokea Real Sociedad na ujio wake ndani ya Manchester City umefungua milango kwa mlinda mlango wa klabu hiyo Joe Hart kutimka.
Bravo anakuwa mchezaji wa nane kujiunga na Manchester City tangu klabu hiyo ilipoanzwa kufundishwa na Pep Guardiola baada ya Ilkay Gundogan, Aaron Mooy, Nolito, Oleksandr Zinchenko, Leroy Sane, Gabriel Jesus na Marlos Moreno.
0 comments:
Post a Comment