Barcelona, Hispania.
BARCELONA imezianza mapema fujo za kuutetea ubingwa wake wa La Liga iliyoutwaa msimu uliopita baada ya usiku huu kuibamiza Real Betis kwa mabao 6-2 katika mchezo safi ulichezwa katika dimba la Uwanja wa Camp Nou,Barcelona.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez aliyefunga mabao matatu (hat-trick) (42' , 56 ',82 '),Lionel Messi aliyefunga mabao mawili (37,57) na Arda Turan aliyefunga bao moja (6)'.
Mabao yote mawili ya Real Betis yamefungwa na Ruben Castro katika kipindi cha kwanza na cha pili (21,84)
0 comments:
Post a Comment