Rio de Janeiro,Brazil.
BAADA ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Brazil cha wachezaji waliochini ya umri wa miaka 23 kutwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki kwa mara ya kwanza katika historia,Neymar Jr,ametangaza kujiuzulu wadhifa wake wa unahodha katika kikosi hicho.
Akifanya mahojiano na kituo cha SporTV mara baada ya kuiongoza Brazil kuilaza Ujerumani kwa penati 5-4 katika mchezo wa fainali Jumamosi Usiku,Neymar Jr amesema
"Ilikuwa ni heshima kubwa kuwa nahodha lakini kuanzia leo mimi siyo nahodha tena.Nautuma ujumbe huu kwa Tite [Kocha mpya wa Brazil] atafute nahodha mpya."
Neymar Jr alichaguliwa kuwa nahodha wa Brazil Septemba 2014 na aliyekuwa kocha mkuu wa wakati huo,Carlos Dunga,aliyekuwa amechukua nafasi ya kocha Felipe Scolari aliyekuwa ametimuliwa kibarua chake baada ya kufanya vibaya katika fainali za kombe la dunia la mwaka huo.
0 comments:
Post a Comment