728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 26, 2016

    MABADILIKO,LIGI NNE ZA ULAYA ZAONGEZEWA NAFASI LIGI YA MABINGWA WA ULAYA (UCL).


    Monaco,Ufaransa.

    Ligi nne kuu za mataifa ya Ulaya zinazoongoza zitatengewa nafasi nne kila moja katika hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuanzia msimu wa 2018-19.

    Ligi hizo ni za England, Ujerumani, Italia na Uhispania.

    Katika mfumo wa sasa,England,Ujerumani na Uhispania huwa na nafasi tatu, huku klabu zinazomaliza katika nafasi ya nne zikilazimika kucheza hatua ya mtoano wa kabla ya makundi.

    Italia imekuwa na nafasi mbili pekee za uhakika, na nyingine moja ya kufuzu kabla ya hatua ya makundi.

    Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashindano wa Uefa Giorgio Marchetti, mpangilio wa Ligi ya Mabingwa hata hivyo utabaki vilevile.

    Baada ya hatua ya kufuzu, klabu 32 zitapangwa katika makundi manane ya klabu nne ambazo zitapigania nafasi ya kuingia hatua ya mtoano ya klabu 16.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MABADILIKO,LIGI NNE ZA ULAYA ZAONGEZEWA NAFASI LIGI YA MABINGWA WA ULAYA (UCL). Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top