Manchester, Uingereza.
MANCHESTER City imetinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya usiku huu kuifunga Steaua Bucharest ya Romania kwa jumla ya bao 1-0 katika mchezo wa marudiano wa hatua ya mtoano uliochezwa katika uwanja wa Etihad jijini Manchester.
Bao pekee la mchezo huo ambao ulishuhudia mlinda mlango Joe Hart akianza kikosi cha kwanza msimu huu limefungwa dakika ya 56 kwa kichwa na Kiungo, Fabian Delph,akimalizia krosi safi kutoka kwa Jesus Navas na kuifanya Manchester City ihitimishe hatua ya mtoano kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-0.
Katika mchezo wa awali uliochezwa Bucharest,Romania wiki iliyopita Manchester City ilishinda kwa mabao 5-0.
0 comments:
Post a Comment