Stoke,Uingereza.
MANCHESTER CITY City imekalia kiti cha uongozi wa msimamo wa ligi kuu England baada ya mchana wa leo kuitandika Stoke City kwa mabao 4-1 katika mchezo wa mapema uliochezwa katika uwanja wa Bet365 Stadium.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na Sergio Aguaro dakika za 27 kwa mkwaju wa penati na dakika ya 36 kwa kichwa.
Mabao mengine ya Manchester City yamefungwa na Manuel Arago Nolito dakika za 86 na 90.Bao la Stoke City limefungwa na Bojan Krkic kwa mkwaju wa penati dakika ya 49.
Ushindi huo umeifanya Manchester City ifikishe pointi sita na kukalia kiti cha uongozi.
0 comments:
Post a Comment