London,England.
Klabu ya Crystal Palace imevunja rekodi yake ya usajili baada ya leo mchana kumsajili mshambuliaji,Mbelgiji Christian Benteke,kutoka klabu ya Liverpool kwa ada ya £27m.
Benteke,25,amesaini mkataba wamiakka minne wa kuitumikia Crystal Palace baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Benteke alijiunga na Liverpool msimu uliopita akitokea Aston Villa kwa ada ya £32.5m lakini kutokana na kuwa majeruhi wa mara kwa mara alijikuta akiwa mshambuliaji chaguo la tatu nyuma ya Divock Origi na Roberto Firmino.
Benteke ameihama Liverpool baada ya kuifungia mabao 10 katika michezo 42.
0 comments:
Post a Comment