Leceister,Uingereza.
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Algeria,Islam Slimani,akiwa ameshika jezi ya Leceister City baada ya kukamilisha usajili wa £30m kutoka Sporting Lisbon ya Ureno.
Slimani,28,amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Leceister City na anakuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu hiyo.
Msimu uliopita Slimani aliifungia Sporting Lisbon mabao 27 katika michezo 33 ya ligi kuu nchini Ureno.Pia ameifungia Algeria mabao 23 katika michezo 43.
0 comments:
Post a Comment