728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 21, 2016

    SERENGETI BOYS YAIGONGA AMAJIMBOS 2-0 CHAMAZI NA KUKARIBIA KUFUZU AFCON


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za Afrika mwakani nchini Madagascar, baada ya jioni ya leo kuifunga Afrika Kusini mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi,Dar Es Salaam.

    Mabao yaliyoipa ushindi huo mnono Serengeti Boys yamefungwa na Mohamed Rashid Abdallah dakika ya 36 na Muhsin Malima Makame dakika ya 85.Katika mchezo wa awali uliochezwa huko Afrika Kusini wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

    Serengeti Boys sasa itavaana na mshindi kati ya Congo Brazaville na Namibia kabla ya kujihakikishia kufuzu fainali za michezo ya AFCON ya vijana mwakani nchini Madagascar.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAIGONGA AMAJIMBOS 2-0 CHAMAZI NA KUKARIBIA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top