728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 23, 2016

    YANGA SC YAHITIMISHA NANE BORA KWA KICHAPO


    Lubumbashi,Congo.

    YANGA SC imehitimisha rasmi michezo yake ya kombe la shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo kukubali kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo mkali wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Stade de Frederic Kibassa Maliba,Lubumbashi.

    Yanga SC ambayo ilimpoteza beki wake Vincent Andrew Dante aliyelimwa kadi nyekundu dakika ya 30 ilijikuta ikiruhusu bao lililofungwa Jonathan Bolingi dakika ya 28.

    Rainford Kalaba aliiandikia TP Mazembe mabao mengine mawili dakika za 55 na 65 kabla ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga SC bao la kufutia machozi dakika ya 75.

    Matokeo hayo yameifanya TP Mazembe ibaki kileleni mwa msimamo wa kundi A baada ya kufikisha alama 13.Yanga SC imebaki mkiani na alama zake nne baada ya kushuka dimbani mara sita.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAHITIMISHA NANE BORA KWA KICHAPO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top