728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 27, 2016

    BAYERN MUNICH YAANZA BUNDESLIGA KIBABE YAICHAPA WEDER BREMEN 6-0,LEWANDOWSKI APIGA 3


    Munich,Ujerumani.

    Robert Lewandowski amefunga hat-trick ya pili ndani ya siku nane na kuiwezesha Bayern Munich kuuanza msimu mpya wa ligi ya bundesliga kwa kishindo kikubwa baada ya Ijumaa usiku kuichapa Werder Bremen kwa jumla ya mabao 6-0 nyumbani Allianz Arena.

    Lewandowski ambaye alifunga hat-trick Ijumaa iliyopita katika ushindi wa Bayern Munich wa mabao 5-0 dhidi ya Carl Zeiss Jena katika michuano ya DFB-Pokal amerudia tena hilo jana ambapo ligi ya Bundesliga ilikuwa inafikisha msimu wake wa 54 tangu ilipoasisiwa.

    Xabi Alonso ndiye aliyeanza kufungua ukurasa wa mabao baada ya kufunga bao safi dakika ya 9 ya kipindi cha kwanza kabla ya Lewandowski kuongeza mawili dakika ya 13 na 46 na kufanya Bayern Munich iende mapumziko ikiwa kifua mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.

    Kipindi cha pili Philip Lahm na Frank Ribery waliifungia Bayern Munich bao la nne na la tano dakika za 66 na 73 kabla  ya Lewandowski kuifunga bao la sita kwa mkwaju wa penati dakika ya 77 baada ya Maximilian Eggestein wa Weder Bremen kumchezea madhambi Rafinha.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAYERN MUNICH YAANZA BUNDESLIGA KIBABE YAICHAPA WEDER BREMEN 6-0,LEWANDOWSKI APIGA 3 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top