Istanbul, Uturuki.
NDOTO ya kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Cheick Ismael Tiote,kuihama Newcastle United imeingia mdudu baada ya kufeli vipimo vya afya katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki.
Tiote,30,ambaye jana usiku aliwasili katika jiji la Istanbul na kulakiwa na mashabiki lukuki wa Galatasaray amegundulika kuwa na tatizo katika mguu wake wa kushoto.
Taarifa kutoka katika vyombo vya habari vya Uturuki vya AmkSpor, NtvSpor na Milliyet zimesema timu ya madaktari wa Galatasaray imegundua kuwa mguu wa kushoto wa Tiote ni dhaifu sana kutokana na madhara ya majeruhi aliyokuwa amejapata siku za nyuma.
Wakati huohuo taarifa nyingine kutoka Uturuki zinasema Galatasaray imeiagiza timu yake ya madaktari kuandaa ripoti ya kina juu ya tatizo la kiungo huyo wa ulinzi.
Galatasaray pia imeagiza ipewe taarifa juu ya muda ambao tatizo hilo litachukua ili kupona vyema kabla haijamua kuendelea ama kuachana na usajili huo ambao utaigharimu £1.2m.
0 comments:
Post a Comment