Hull,Uingereza.
MARCUS Rashford amefunga bao moja na kuiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Hull City katika mchezo mgumu uliochezwa katika uwanja wa KCOM Stadium.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi,John Moss,Marco Rashford alifunga bao hilo la pekee dakika ya 92 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa nahodha,Wayne Rooney.
Matokeo hayo yameifanya Manchester United ijikusanyie pointi tisa baada ya kushuka dimbani mara tatu na sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi nyuma ya Chelsea iliyo kileleni.
0 comments:
Post a Comment