Genk,Ubelgiji.
MBWANA Samatta amefunga bao moja na kuiwezesha klabu yake ya KRC Genk kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Europa Ligi baada ya usiku huu kuichapa NK Lokomotiva kwa mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa katika uwanja wa Cristal Arena jijini Genk.
Samatta alianza kuifungia KRC Genk dakika ya kwanza ya kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri ya Leon Bailey.
Bao la pili limefungwa na Leon Bailey dakika ya 50 ya kipindi cha pili cha mchezo baada ya kupokea pasi ya Leandro Trossard.
Matokeo hayo yameifanya KRC Genk iweze kufuzu kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya mchezo wa awali timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.
0 comments:
Post a Comment