Manchester, Uingereza.
Raheem Sterling amefunga mabao mawili na kuiwezesha Manchester City kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Westham United katika uwanja wa Etihad ulioko jijini Manchester.
Bao jingine la Manchester City limefungwa na Fernandisho huku lile la Westham United likifungwa kwa kichwa na Michael Antonio.
Ushindi huo ambao ni wa tatu umeifanya Manchester City ifikishe pointi tisa huku Westham United ikibaki na pointi zake tatu baada ya kuambulia ushindi katika mchezo mmoja peke yake.
Ligi kuu Uingereza itaendelea tena Jumamosi ya Septemba 10 mwaka huu kupisha michezo ya kimataifa itakayopigwa wikendi ijayo.
0 comments:
Post a Comment