Zagreb,Croatia.
KIUNGO wa Real Madrid Luka Modric ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Croatia na Kocha wa nchi hiyo Ante Cacic.
Uwamuzi wa kumteua Modric mwenye umri wa miaka 30 sasa umekuja baada ya aliyekuwa nahodha wa siku nyingi wa timu hiyo Darijo Srna kujiuzulu.
Modric ataanza jukumu hilo jipya Septemba 5 katika mchezo ambao Croatia itakuwa nyumbani Zagreb kuiaalika Uturuki katika mchezo wa kundi I wa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia.
Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na mgumu utachezwa bila ya mashabiki.Mashabiki wa Croatia wamepigwa marufuku kuushuhudia mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha za kibaguzi kwa wachezaji wageni.
Timu nyingine zilizopo katika kundi hilo la I ni Ukraine,Iceland,Finland na Kosovo.
0 comments:
Post a Comment