Manchester, Uingereza.
KIUNGO wa Manchester United,Mjerumani Bastian Schweinsteiger,amefichua kwamba klabu hiyo yenye maskani yake katika dimba la Old Trafford ndiyo itakayokuwa ya mwisho kuichezea barani Ulaya na siyo vinginevyo.
Schweinsteiger,32,amefichua hilo mchana wa leo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya kuwepo kwa uvumi kwamba anafikiria kuihama Manchester United na kujiunga na klabu nyingine za Ulaya ikiwemo Galatasaray ya Uturuki.
Schweinsteiger ambaye bado hajapata nafasi ya kuichezea Manchester United tangu ilipoanza kunolewa na Mreno Jose Mourinho amesisitiza kuwa kwa sasa yeye bado ni mchezaji wa Manchester United lakini kama ataamua kuhama basi atakwenda kucheza soka nje ya Ulaya.
Ameiambia ESPN FC "MUFC itakuwa klabu yangu ya mwisho Ulaya.Naviheshimu vilabu vingine,lakini Manchester United ndiyo klabu pekee niliyoipa nafasi ya kuniondoa Bayern Munich".
Schweinsteiger alijiunga na Manchester United mwaka 2015 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Bayern Munich aliyoichezea kwa kipindi cha miaka 13 akiisaidia kutwaa vikombe 22 ikiwemo vikombe vinane vya Bundesliga na kimoja cha ligi ya mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment